# Taarifa ya jumla Mistari ya 13-18 inarudia kwa mara ya tatu na kutoa kwa undani kuhusu jinsi gani Nuhu aliingia katika safina pamoja na familia yake na wanyama katika 7:1. Hili si tukio jipya. # Katika siku iyo hiyo "Katika siku hiyo hasa". Hii ina maana ya siku ambayo mvua ilianza kunyesha. Mistari ya 13-16 inaeleza Nuhu alichofanya kabla tu ya mvua kuanza. # mnyama wa mwitu ... mnyama wa kufugwa ... kila kitambaacho ... ndege Vikundi hivi vinne vinaorodheshwa kuonyesha ya kwamba kila aina ya mnyama alijumuishwa. # kila kitambaacho Hii ina maana ya wanyama watambaao juu ya ardhi, kama wanyama wagugunaji, wadudu, mjusi na nyoka. # kwa jinsi yake "ili kwamba kila aina ya mnyama azalishe zaidi ya kila aina yake"