sw_tn/gen/01/06.md

28 lines
972 B
Markdown

# Na kuwe na anga kati ya maji ...na ligawe
Hizi ni amri. Kwa kuamuru kwamba anga kati ya maji iwepo na igawe maji, Mungu alifanya iwepo na kugawa maji na maji.
# anga
"anga tupu na wazi". Watu wa Kiyahudi walichukulia uwazi huu kuwa na umbo kama la kuba au bakuli lililofunikwa.
# kati ya maji
"ndani ya maji"
# Mungu alifanya anga na kugawanya maji
"kwa namna hii, Mungu alifanya anga na kugawa maji." Mungu alipozungumza, ilitokea. Sentensi hii inaeleza kitu gani Mungu alifanya alipokuwa akizungumza.
# ikawa hivyo
"ilitokea kama hivyo" au "Hivyo ndivyo ilivyotokea". Mungu alichoamuru kilitokea kama alivyotamka kitokee. Msemo huu hujitokeza katika sura nzima na una maana ile ile kila unapojitokeza.
# jioni na asubuhi
Hii inamaanisha siku nzima. Mwandishi anazungumzia siku nzima kana kwamba ni sehemu mbili. Kwa tamaduni za Kiyahudi, siku moja huanza baada ya jua kuzama.
# siku ya pili
Hii inamaanisha siku ya pili ambapo ulimwengu ulipoanza kuwepo.