sw_tn/ezk/33/21.md

1.0 KiB

katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa kumi

Huu ni mwezi wa kumi wa kalenda ya Kiebrania. Siku ya kumi na tano ni karibu na mwanzoni mwa Mwezi wa kwanza katika kalenda za Magahribi.

mateka wetu

Hapa "wetu" inarejea kwa Ezekieli na Waisraeli ambao walikuwa katika Babeli tangu wakati Wababeli walipomlazimisha Mfalme Yehoyakini kuondoka Yerusalemu.

mtu mmoja akatoroka kutoka Yerusalemuna

"mtu mmoja alitoroka kutoka Yerusalemu na kuja kwangu." Wababeli waliiangamiza Yerusalemu na kuwaua watu wa Yerusalemu, lakini watu walikimbia.

Mji ulikuwa umetekwa

"Wababeli wameuangamiza mji." Neno "mji" linairejea "Yerusalemu."

Mkono wa Yahwe ulikuwa juu yangu

Tazama tafsiri yake katika sura ya 1:1, "mkono wa Yahwe ulikuja juu yangu."

mapambazuko

"Mapambazuko" ni mda wa asubuhi sana wakati mwanga wa jua unapoanza kuchomoza.

kinywa changu kilifunuliwa

"Yahwe alifungua kinywa chake." "nitafungua kinywa chako"

sikuwa bubu tena

"niliweza kuzungumza sasa" Ezekieli hakuweza kuzungumza chochote isipokuwa maneno ya kinabii tangu 3:26.