sw_tn/ezk/21/06.md

906 B

Maelezo ya Jumla:

Yahwe ananena na Ezekieli.

mwana wa adamu

"mwana wa mwanadamu"

gumia kama kuvunjika kwa viuno vyako

Yahwe anamwambia Ezekieli kugugumia kama ishara ya kuusindikiza ujumbe wake. Anamwambia kugugumia kwa kina kana kwamba tumbo lake lilikuwa kwenye maumivu makubwa sana.

Katika uchungu wa gumia

"Kwa huzuni kubwa"

mbele ya macho yao

Hapa Waisraeli wanarejelewa kwa "macho" yao kusisitiza kile wakionacho. "mbele yao" au "mbele ya watu wa Israeli"

ile habari inayokuja

Hii inazungumzia "habari" kana kwamba ilikuwa mtu ambaye alikuwa akija kwao punde.

kwa kila moyo utakaozimia

Hii inazungumzia watu kuogopa kana kwamba mioyo yao ilikuwa ikizimia.

utasita

"utakuwa dhaifu"

Kila roho itazimia

Hii inazungumzia watu kuwa na hofu katika roho zao kana kwamba roho zao zilitaka kuzimia.

kila goti litatiririka kama maji

"kila goti litakuwa dhaifu kama maji"