sw_tn/eph/05/25.md

1.1 KiB

wapendeni wake zenu

Hapa "pendo" linarejea pasipo ubinafsi, kutumika, au kutoa upendo.

kujitoa mwenyewe kwaajili yake, kwamba unaweza kumfanya yeye mtakatifu kwasababu yeye alitusafisha sisi

Maneno "mwenyewe" na "yeye" yanarejea kwa Kristo. Maneno "yeye" na "sisi" yanarejea kwa Kanisa.

kajitoa mwenyewe kwaajili yake

NI: "Kristo alitoa kila kitu kwaajili yake"

yeye alitusafisha sisi kwa kutuosha kwa maji kupitia neno

Maana zinazowezekana ni 1) Paulo anarejea kuwa umekuwa ukisafishwa kwa neno la Mungu na kupitia ubatizo wa maji katika Kristo au 2) Paulo anasema Mungu alitufanya sisi wasafi kiroho kutoka katika dhambi zetu kwa neno la Mungu kama tunavyoifanya miili yetu safi kwa kuiosha kwa maji.

kwamba yeye aweza kujiwasilishia mwenyewe kanisa

"kwamba anaweza kuwasilisha kwake mwenyewe kanisa"

bila waa au kunyanzi

Paulo anasema kuhusu Kanisa kama vazi ambalo ni safi na liko katika hali nzuri. Anatumia wazo lile lile katika namna mbili kusisitiza utakatifu wa Kanisa.

takatifu na bila makosa

Kauli "bila makosa" kimsingi inamaanisha kitu kile kile "mtakatifu." Paulo anatumia viwili pamoja kusisitiza utakatifu wa kanisa.