sw_tn/eph/04/01.md

738 B

kauli unganishi

Kwasababu ya kile Paulo amekuwa akiwaandikia Waefeso, anawatia moyo namna gani kuishi maisha yao kama waamini na tena anasisitiza umoja wa waamini.

Kama mfungwa kwa ajili ya Bwana

"kama mtu ambaye yuko gerezani kwa sababu ya uchaguzi wake wa kumtumikia Bwana"

Nawasihi ninyi kuishi maisha yanayoendana na wito

Neno "ninyi" linamaanisha Waefeso waamini. AT: "Nawatia moyo ninyi kujitunza wenyewe kwa namna nzuri ya wito."

Kwa unyenyekevu mkubwa na upole na uvumilivu, mkichukuliana kila mmoja katika upendo

"jifunzeni kuwa wanyenyekevu, wapole, waumilivu na kuchukuliana kila mmoja katika upendo"

Tunzeni umoja wa Roho katika kifungo cha amani

"tafuteni kuishi pamoja kwa amani kuuhifadhi umoja wa Roho"