sw_tn/eph/02/17.md

778 B

Maelezo au Sentensi Unganishi.

Paulo anawaambia waamini wakiefeso kwamba watu wa mataifa walioamini wamefanyika wamoja na mitume na manabii, na ni hekalu kwa Mungu katika Roho Mtakatifu.

amani iliyotangazwa

Tasfiri mbadala: "injili ya amani iliyotangazwa" au "injili ya amani iliyotangazwa kwa uwazi"

ninyi mliokuwa mbali

Hii inazungumzia juu ya watu wa mataifa au wale wasio Wayahudi.

wale waliokuwa karibu

Hii inazungumzia juu ya Wayahudi.

Kwa maana kwa njia ya Yesu sisi sote wawili tuna nafasi.

Hapa "sisi sote wawili" inazungumzia juu ya Paulo, waamini wa Kiyahudi na waamini wasio Wayahudi.

kwa yule Roho Mtakatifu

Waamini wote, yaani Wayahudi na watu wa mataifa, wamepewa haki ya kuingia mbele za uwepo wa Mungu Baba kwa Roho Mtakatifu yule yule.