sw_tn/eph/02/17.md

24 lines
778 B
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2018-04-12 01:01:04 +00:00
# Maelezo au Sentensi Unganishi.
Paulo anawaambia waamini wakiefeso kwamba watu wa mataifa walioamini wamefanyika wamoja na mitume na manabii, na ni hekalu kwa Mungu katika Roho Mtakatifu.
# amani iliyotangazwa
Tasfiri mbadala: "injili ya amani iliyotangazwa" au "injili ya amani iliyotangazwa kwa uwazi"
# ninyi mliokuwa mbali
Hii inazungumzia juu ya watu wa mataifa au wale wasio Wayahudi.
# wale waliokuwa karibu
Hii inazungumzia juu ya Wayahudi.
# Kwa maana kwa njia ya Yesu sisi sote wawili tuna nafasi.
Hapa "sisi sote wawili" inazungumzia juu ya Paulo, waamini wa Kiyahudi na waamini wasio Wayahudi.
# kwa yule Roho Mtakatifu
Waamini wote, yaani Wayahudi na watu wa mataifa, wamepewa haki ya kuingia mbele za uwepo wa Mungu Baba kwa Roho Mtakatifu yule yule.