sw_tn/eph/02/13.md

48 lines
1.5 KiB
Markdown

# Sasa katika Kristo Yesu
Paulo anawatofautisha Waefeso kabla ya kumwamini Kirsto na baada ya kumwamini Kristo
# ninyi ambao hapo mwanzo mlikuwa mbali na Mungu, mmeletwa karibu na Mungu
Kwa sababu ya dhambi za waamini, walikuwa wametengwa na Mungu. Hata hivyo, sasa Yesu amewaleta karibu na Mungu kwa damu yake.
# yeye ndiye amani yetu
Tafsiri mbadala: "Yesu hutupa amani yake"
# Kwa mwili wake
Tafsiri mbadala: "Kwa kifo chake juu ya msalaba"
# ukuta wa utenganisho
Tafsiri mbadala: "ukuta wa chuki" au "nia mbaya"
# umetutenganisha
Herufi za kwanza "ume" zinaelezea kwamba huo ukuta uliwatenganisha wote Paulo na Waefeso, ambao uliwatenga waumini wa Kiyahudi kutoka kwa waumini wasiokuwa Wakiyahudi (wamataifa)
# aliiondoa sheria ya amri na kanuni
Damu ya Yesu ilileta utoshelevu wa sheria ya Musa ili kwamba wote Wayahudi na watu wa mataifa wanaweza kuishi kwa amani ndani ya Mungu.
# mtu mmoja mpya
Mtu mmoja mpya, mtu wa jamii ya watu waliokombolewa.
# ndani yake
Ni muunganiko na Yesu ambao unafanya upatanisho uwezekane kati ya Wayahudi na watu wa mataifa.
# kuwapatanisha watu wote
Tafsiri mbadala: "kuwaleta pamoja wote wawili yaani Wayahudi na watu wa Mataifa (wamataifa)"
# kupitia msalaba...kwa njia ya msalaba
Hii ni kwamba, kwa njia ya Kifo cha Kristo juu ya msalaba.
# aliufisha (aliuua) uadui kwa msalaba
Yesu aliondoa kabisa sababu ambayo iliwafanya Wayahudi na watu wa mataifa kuwa maadui. Hawakuhitajika tena kuishi kulingana na sheria ya Musa.