# Sasa katika Kristo Yesu Paulo anawatofautisha Waefeso kabla ya kumwamini Kirsto na baada ya kumwamini Kristo # ninyi ambao hapo mwanzo mlikuwa mbali na Mungu, mmeletwa karibu na Mungu Kwa sababu ya dhambi za waamini, walikuwa wametengwa na Mungu. Hata hivyo, sasa Yesu amewaleta karibu na Mungu kwa damu yake. # yeye ndiye amani yetu Tafsiri mbadala: "Yesu hutupa amani yake" # Kwa mwili wake Tafsiri mbadala: "Kwa kifo chake juu ya msalaba" # ukuta wa utenganisho Tafsiri mbadala: "ukuta wa chuki" au "nia mbaya" # umetutenganisha Herufi za kwanza "ume" zinaelezea kwamba huo ukuta uliwatenganisha wote Paulo na Waefeso, ambao uliwatenga waumini wa Kiyahudi kutoka kwa waumini wasiokuwa Wakiyahudi (wamataifa) # aliiondoa sheria ya amri na kanuni Damu ya Yesu ilileta utoshelevu wa sheria ya Musa ili kwamba wote Wayahudi na watu wa mataifa wanaweza kuishi kwa amani ndani ya Mungu. # mtu mmoja mpya Mtu mmoja mpya, mtu wa jamii ya watu waliokombolewa. # ndani yake Ni muunganiko na Yesu ambao unafanya upatanisho uwezekane kati ya Wayahudi na watu wa mataifa. # kuwapatanisha watu wote Tafsiri mbadala: "kuwaleta pamoja wote wawili yaani Wayahudi na watu wa Mataifa (wamataifa)" # kupitia msalaba...kwa njia ya msalaba Hii ni kwamba, kwa njia ya Kifo cha Kristo juu ya msalaba. # aliufisha (aliuua) uadui kwa msalaba Yesu aliondoa kabisa sababu ambayo iliwafanya Wayahudi na watu wa mataifa kuwa maadui. Hawakuhitajika tena kuishi kulingana na sheria ya Musa.