sw_tn/deu/32/30.md

1.2 KiB

Taarifa ya Jumla:

Musa anazungumzia wimbo wa shairi kwa watu wa Israeli. Anaendela kunukuu maneno ya Yahwe na kuwaambia zaidi ya yale waliyopaswa kuelewa iwapo wangekuwa na hekima (32:28).

Inawezekanaje mmoja kufukuza maelfu ... Yahwe hajawaachilia kwao?

Musa anatumia swali kukaripia watu kwa kutokuwa na hekima ya kutosha kuelewa kwa nini adui zao wanawashinda. Swali hili linaweza kutafsiriwa kama kauli.

Inawezekanaje mmoja kufukuza maelfu, na wawili kuweka makumi elfu mbioni

Unaweza kuweka wazi taarifa inayoeleweka. "Inawezekanaje askari adui mmoja kufukuza wanamume 1,000, na maaskari wawili adui kusababisha wanamume wako 10,000 kukimbia"

isipokuwa Mwamba wao hajawauza

Neno la "Mwamba" lina maana ya Yahwe amnaye ana nguvu na anaweza kulinda watu wake. "isipokuwa Yahwe, Mwamba wao, asingewapa kwao"

Mwamba wao ... Mwamba wetu

"Mwamba" ni jina stahiki ambalo Musa anamptia Yakwe, ambaye, kama mwamba, ana nguvu na anaweza kulinda watu wake.

mwamba wa maadui zetu si kama Mwamba wetu

Sanamu za maadui na miungu ya uongo havina nguvu kama za Yahwe.

kama vile maadui zetu wanavyokiri

"sio tu hatusemi hivyo, lakni adui wetu wanasema hivyo pia"