sw_tn/deu/32/07.md

1.0 KiB

Taarifa ya Jumla:

Musa anazungumza wimbo wa shairi kwa watu wa Israeli.

Kumbukeni ... tafakari ... baba yako ... atakuonyesha ... wazee wako ... watakuambia

Musa anazungumza na watu wa Israeli kana kwamba walikuwa mtu mmoja, kwa hiyo neno "yako" hapa ni katika umoja.

Kumbukeni

Hii ni lahaja. "Kumbuka"

siku zile za zamani

"siku za zamani". Musa ana maana ya kipindi ambapo mababu wa watu wa Israeli walikuwa hai.

tafakari juu ya miaka mingi ya nyuma

Haya ni marudio ya kile ambacho Musa amemaliza kusema katika sehemu iliyopita. Musa anataka watu wa Israeli kulenga historia yao kama taifa.

atakuonyesha

"atafanya iwe wazi kwako" au "atakuwezesha kuelewa"

alipowapatia mataifa urithi wao

Hii ni lahaja. "kuweka mataifa katika sehemu ambazo wangeishi". Maneno yanayofanana, "kuwapatia kama urithi," inajitokeza katika 4:21.

na kuweka mipaka ya watu, na alipoimarisha idadi ya miungu yao

Mungu aliwapa kila kundi la watu, pamoja na miungu yao, eneo lake mwenyewe. Kwa njia hii, alipunguza ushawishi wa miungu ya kundi la watu.