sw_tn/deu/30/19.md

1.0 KiB
Raw Permalink Blame History

Taarifa ya Jumla:

Musa anaongea na Waisraeli kana kwamba walikuwa mtu mmoja, isipokuwa pale inapoandikwa neno "yako" ni katika umoja.

Naziita mbingu na nchi kushuhudia

Maana zaweza kuwa 1) Musa anawaita wale wanaoishi mbinguni na duniani kwa mashahidi kwa kile anachosema, au 2) Musa anazungumza kwa mbingu na dunia kana kwamba ni watu, na kuziita kama mahsahidi kwa kile anachosema.

kushuhudia dhidi yako

"kuwa tayari kusema ya kwamba umefanya mambo maovu"

dhidi yako leo

Musa anazungumza na Waisraeli kama kundi.

kutii sauti yake

Hapa "sauti" ina maana ya kile Yahwe alischosema. "tii kile anachosema"

na kungangania kwake

"na kumtegemea yey"

Kwa maana yeye ni uzima wako na urefu wa siku zako

"Uzima wako" na "urefu wa siku zako" ni lugha nyingine kwa yule ambaye hutoa uhai na urefu wa siku. Unaweza kuunganisha misemo hii miwili ukihitaji. "Yahwe ni yeye pekee anayeweza kukuwezesha kuishi maisha marefu"

aliapa kwa mababu zako

udondoshaji wa maneno unaweza kujazwa. "aliapa ya kwamba angewapa mababu zako"