sw_tn/deu/29/02.md

1.0 KiB

Mmeona kila kitu ambacho Yahwe alifanya mbele ya macho yenu

Hapa "macho" yanasisitiza ya kwamba Yahwe alitarajia wao kukumbuka ya kwamba walikiona. "Mmeona yote ambayo Yahwe alifanya ili kwamba muone na kukumbuka alichofanya"

mateso makubwa ambayo macho yenu yaliona

Hapa "macho" yanasisitiza ya kwamba Yahwe alitarajia wao kukumbuka ya kwamba walikiona. "mmeona wenyewe ya kwamba watu waliteseka vibaya"

macho yako

Musa anazungumza na Waisraeli kana kwamba walikuwa mtu mmoja, kwa hiyo neno "yako" hapa ni katika umoja.

ishara, pamoja na ile miujiza mikubwa

Maneno "ishara" na "miujiza" yote ina maana ya mapigo ambayo Yahwe alituma juu ya Misri. "na vitu vyote vyenye uwezo ambavyo Yahwe alifanya"

Yahwe hajawapatia moyo wa kufahamu, macho ya kuona, au masikio ya kusikia

Watu wana mioyo, macho, na masikio. Lugha hii inasema ya kwamba Yahwe hajawawezesha kuelewa kile walichokiona na kusikia kutoka kwa Yahwe, na kwa nini na namna gani wanapaswa kumtii"

hajawapatia moyo wa kufahamu

Hii ni lahaja. "kuwawezesha kuelewa"