sw_tn/deu/24/12.md

923 B

Taarifa ya Jumla:

Musa anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli kana kwamba walikuwa mtu mmoja, kwa hiyo neno "yako" hapa ni katika umoja.

hautakiwi kulala na dhamana yake ikiwa mikononi mwako

"Hautakiwi kubaki na koti lake usiku wote"

dhamana yake

Hii ni lugha nyingine ya "kile alichoahidi angefanya kutoa kama angeshindwa kulipa kile alichokopa"

kumrejeshea dhamana yake

"umrudishie alichokupatia kukuonyesha ya kwamba atalipa mkopo wake"

ili aweze kulala ndani ya vazi lake na akubariki

Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "ili kwamba aweze kuwa na koti lake kujipatia joto anapolala, na kuwa na shukurani kwako"

vazi

Koti au nguo nyingine ambayo humpatia mtu joto wakati wa usiku. Yawezekana hii ilikuwa "dhamana" ambayo Musa alikuwa akizungumzia katika 24:10.

itakuwa utakatifu kwako mbele za Yahwe Mungu wako

"Yahwe Mungu wako atatoa kibali kwa jinsi ulivyosimamia suala hili"