sw_tn/dan/12/05.md

968 B

Maelezo ya jumla

Malaika amemaliza kuongea, na Danieli anaendelea kusema kile alichokiona baadaye katika maono yake tangu katika 10:4

kulikuwa na malaika wengine wawili wamesimama

"kulikuwa na malaika wengine wawili wamesimama"

Mmoja wao alimwambia mtu aliyevaa nguo za kitani,

Hii inamrejelea mtu aliyekuwa akiongea na Danieli, siyo mmoja wale watu waliokuwa wamesimama pembeni mwa mtu.

ukingo wa mto,

Maana zinazoweza kukubalika 1) malaika alikuwa juu ya mto au 2) malaika alikuwa mbali katika ukingo sambamba na mto.

Je itachukua muda gani mpaka mwisho wa matukio haya ya kushangaza?

"Matukio haya ya kushangaza yatadumu kwa muda gani?" Hii inarejelea mwanzo hadi mwisho wa matukio.

matukio haya ya kushangaza

Katika muda ule ambao malaika alikuwa akiongea na Danieli, hakuna hata tukio hata moja lilikuwa limetokea. Hii kwa uhalisia inarejelea matukio katika 12:1, na huenda yalijumuisha matukio yaliyo katika maono kutoka sura ya 11.