sw_tn/dan/10/04.md

36 lines
1.0 KiB
Markdown

# 4Katika siku ya ishirini na nne ya mwezi wa kwanza,
Huu ni mwezi wa kwanza wa kalenda ya Kiebrania. Siku ya ishirini na nne iko karibu na katikati ya mwezi wa Aprili matika kalenda ya Magharibi.
# akiwa na mkanda kiunoni mwake
"na alikuwa amevaa mkanda"
# Ufazi
Ufazi ni sehemu. sehemu yake haijulikanai.
# Mwili wake ulikuwa kama kito
Mwlii wake uling'ara kwa mwanga wa bluu na njano kana kwamba ulikuwa umetengenezwa kwa kito.
# kito
jiwe la thamani lenye rangi ya bluu au njano.
# na sura yake ilikuwa kama radi
Sura yake iling'aa kama mwali wa radi unavyong'ara.
# Macho yake yalikuwa kama miali ya tochi
Macho yake yalikuwa yanang'aa kwa mwanga kana kwamba yalikuwa miali ya tochi.
# mikono yake na miguu yake ilikuwa kama shaba iliyosafishwa
Mikono yake na miguu yake ilikuwa iking'aa kana kwamba ilikuwa imetengenezwa kwa shaba iliyosafishwa.
# Sauti ya maneno yake ilikuwa kama sauti ya umati mkubwa wa watu
Sauti yake ilikuwa na nguvu sana kwamba ilikuwa ni kundi kubwa la watu wengi likiongea kwa sauti ya juu.