sw_tn/dan/06/26.md

897 B

Maelezo kiunganishi

Hii inaendelea kueleza ujumbe ambao Dario aliutuma kwa kila mtu katika ufalme wake.

watetemeka na kumcha

Maneno haya yana maana sawa na yanaweza kuunganishwa. "kutetemeka kwa hofu"

Mungu wa Danieli

"Mungu ambaye Danieli alimwabudu"

kwa kuwa ni Mungu aliye hai na huishi milele

Virai hivi viwili "Mungu aliye hai" na "aishiye milele" vinaelezea dhana moja, kwamba Mungu huishi milele.

ufalme wake ha....; utawala wake uta..

Virai hivi vyote viko sambasamba, na vinatia nguvu juuu ya jinsi ufalme wa Mungu hautakuwa na mwisho."

ufalme wake hauwezi kuharibiwa

Maneno haya yaweza kuelezwa katika muundo tendaji. " hakuna yeyote aweza kuuangusha ufalme wake" au "ufalme wake utadumu milele"

utawala wake utakuwepo hadi mwisho.

"atatawala milele"

amemhifadhi Danieli salama dhidi ya uwezo wa simba.

"hajawaruhusu simba wenye nguvu kumdhuru Danieli"