sw_tn/col/02/13.md

1.2 KiB

wakati mlipokuwa mmekufa

"wakati ninyi waumini wa Kolosai mlikuwa mmekufa kiroho"

mlikuwa mmekufa .... aliwafanya kuwa hai

Fumbo hili linaonesha jinsi gani baada ya kutoka katika maisha ya dhambi kwenda maisha mapya ya kiroho ilivyo kama mtu anayefufuka kutoka kifo.

mmekufa katika hatia zenu na kutokutahiriwa kwa miili yenu

mlikuwa mmekufa katika mambo mawili: 1) mlikuwa mmekufa kiroho, mkiishi maisha ya dhambi dhidi ya Kristo na 2) mlikuwa hamkutahiriwa kulingana na sheria ya Musa.

alitusamehe sisi hatia zetu zote

"Yesu Kristo alitusamehe sisi Wayahudi na ninyi watu wa Mataifa makosa yetu yote"

alifuta kumbukumbu za madeni zilizoandikwa na taratibu zilizokuwa kinyume nasi

Fumbo hili hufananisha jinsi ambavyo Mungu anaweza kuondoa dhambi (deni zetu) na kutusamehe sisi kwa kuvunja sheria za Mungu (taratibu) kama ambavyo mtu anaweza kufuta kitu kilichoandikwa kwenye karatasi.

aliwaongoza katika ushindi na milki

Katika kipindi cha Warumi, ilikuwa kawaida kwa jeshi la Kirumi kuwa na "gwaride la ushindi" waliporudi nyumbani, kuonesha wafungwa wote na mali walizoteka.

kwa msalaba

Hapa "msalaba" unasimama bdala ya kifo cha Kristo msalabani.