sw_tn/col/02/08.md

28 lines
1018 B
Markdown

# Sentensi unganishi:
Paulo anawasihi walioamini wawe makini wasigeukie maneno na taratibu za wengine kwa sababu hakuna kinachoweza kuongezeka katika ukamilifu wa Mungu walio nao walioamini katika Kristo.
# Ona kwamba
"Iweni makini kwamba" au "Angalieni kwamba"
# kuwanasa
Paulo anazungumzia vile ambavyo mtu anavyoweza kuamini mafundisho ya uongo (kwa sababu wanaamini mafundisho ya uongo au wanapenda vitu vitu vya uongo)
# falsafa
mafundisho ya kidini na imani yasiyotoka katika neno la Mungu lakini yanatokana na mawazo ya ya watu kuhusu Mungu na maisha
# maneno matupu ya udanganyifu
haya ni mawazo ya upotoshaji ambayo hayatuongozi katika maisha ndani ya Kristo. Hayazalishi chochote; ni matupu au hayana thamani.
# tamaduni za kibinadamu na juu ya mifumo ya dhambi ya dunia
tamaduni zote za Waisraeli na wapagani (watu wa Mataifa) mifumo ya imani haina maana.
# kwa kuwa katika yeye ukamilifu wote wa Mungu unaishi kwa jinsi ya mwili
"kwa sababu asili yote ya Mungu inaishi katika mwili wa Kristo"