# Sentensi unganishi: Paulo anawasihi walioamini wawe makini wasigeukie maneno na taratibu za wengine kwa sababu hakuna kinachoweza kuongezeka katika ukamilifu wa Mungu walio nao walioamini katika Kristo. # Ona kwamba "Iweni makini kwamba" au "Angalieni kwamba" # kuwanasa Paulo anazungumzia vile ambavyo mtu anavyoweza kuamini mafundisho ya uongo (kwa sababu wanaamini mafundisho ya uongo au wanapenda vitu vitu vya uongo) # falsafa mafundisho ya kidini na imani yasiyotoka katika neno la Mungu lakini yanatokana na mawazo ya ya watu kuhusu Mungu na maisha # maneno matupu ya udanganyifu haya ni mawazo ya upotoshaji ambayo hayatuongozi katika maisha ndani ya Kristo. Hayazalishi chochote; ni matupu au hayana thamani. # tamaduni za kibinadamu na juu ya mifumo ya dhambi ya dunia tamaduni zote za Waisraeli na wapagani (watu wa Mataifa) mifumo ya imani haina maana. # kwa kuwa katika yeye ukamilifu wote wa Mungu unaishi kwa jinsi ya mwili "kwa sababu asili yote ya Mungu inaishi katika mwili wa Kristo"