sw_tn/act/19/13.md

36 lines
915 B
Markdown

# Taarifa ya jumla
Huu ni mwanzo wa tukio jingine lililotokea wakati Paulo akiwa Efeso. Ni kuhusu wapunga mapepo Wayahudi.
# Wapunga mapepo
watu ambao hufukuza roho wabaya kutoka kwa watu au maeneo
# akilitumia jina la Yesu kwa matumizi yao wenyewe
Ingawa hawakuwa wakimwamini Yesu, walijaribu kutumia jina lake kama moja ya maneno yao ya muujiza
# Walinena juu yao walikuwa wapegawa na roho chafu
Walilitaja jina la Yesu kwa roho wachafu zilizokuwa zimewapaa watu
# wale waliokuwa na pepo wabaya
wale waliokuwa wakiongozwa na roho wabaya
# Kwa Yesu anayehubiriwa na Paulo
"Yesu" lilikuwa ni jina la kawaida wakati ule, hivyo hao wapunga mapepo waliwataka wato kujua waliyekuwa wakimnena.
# kwa Yesu
Hii inasimamia nguvu na mamlaka ya Yesu.
# Waliofanya vile walikuwa wana saba wa kuhani wa kiyahudi, Skewa.
Hii ni habari inayojadili habari ya wapunga mapepo.
# Skewa
Hili ni jina la mtu mwanaume.