sw_tn/act/09/31.md

40 lines
1.2 KiB
Markdown

# Sentensi unganishi
Katika mstari wa 32, habari inabadirika kutoka simlizi ya Sauli na kuanza simlizi mpya juu ya Petro.
# Maelezo ya jumla
Mstari wa 32 ni habari inayotupatia taarifa za kukua kwa kanisa.
# kanisa lote katika Uyahudi, Galilaya na Samaria
Hapa ni kiwakilishi cha "kanisa" kama umoja likiwakilisha zaidi ya kusanyiko la waumini. Linaelezea waumini wote katika jumuia zote za Israeli.
# lilikuwa na amani
ilikaa kwa amani". Linamaanisha kuwa yale mateso yaliyoanza kwa mauaji ya Stefani yalikuwa yamekoma.
# Likajengwa
Hapa mwezeshaji wake ni "Mungu" au "Roho Mtakatifu". "Mungu aliwasaidia wakue" au "Roho Mtakatifu aliwajenga na kuwa imara".
# Kutembea katika hofu ya Mungu
"waliendelea kumheshimu Bwana'
# Katika faraja ya Roho Mtakatifu
"Roho Mtakatifu aliwaimarisha na kuwapa ujasiri"
# Pande zote za mkoa
Hii ni fahari kwa Petro kutembelea waumini wengi pande za Yuda, Galilaya, na Samaria.
# Alitelemkia
Neno "Alitelemkia" ilieleza kuelekea Lida iliyo upande wa chini kulinganisha na maeneo mengine alikotembelea Petro.
# Lida
Lida ni mji ulioko kati ya kilomita 18 kaskazini mashariki mwa Jafa. Huu mji ulikuwa ukiitwa Lod kwenye Agano la Kale,na katika Israeli ya sasa.