# Sentensi unganishi Katika mstari wa 32, habari inabadirika kutoka simlizi ya Sauli na kuanza simlizi mpya juu ya Petro. # Maelezo ya jumla Mstari wa 32 ni habari inayotupatia taarifa za kukua kwa kanisa. # kanisa lote katika Uyahudi, Galilaya na Samaria Hapa ni kiwakilishi cha "kanisa" kama umoja likiwakilisha zaidi ya kusanyiko la waumini. Linaelezea waumini wote katika jumuia zote za Israeli. # lilikuwa na amani ilikaa kwa amani". Linamaanisha kuwa yale mateso yaliyoanza kwa mauaji ya Stefani yalikuwa yamekoma. # Likajengwa Hapa mwezeshaji wake ni "Mungu" au "Roho Mtakatifu". "Mungu aliwasaidia wakue" au "Roho Mtakatifu aliwajenga na kuwa imara". # Kutembea katika hofu ya Mungu "waliendelea kumheshimu Bwana' # Katika faraja ya Roho Mtakatifu "Roho Mtakatifu aliwaimarisha na kuwapa ujasiri" # Pande zote za mkoa Hii ni fahari kwa Petro kutembelea waumini wengi pande za Yuda, Galilaya, na Samaria. # Alitelemkia Neno "Alitelemkia" ilieleza kuelekea Lida iliyo upande wa chini kulinganisha na maeneo mengine alikotembelea Petro. # Lida Lida ni mji ulioko kati ya kilomita 18 kaskazini mashariki mwa Jafa. Huu mji ulikuwa ukiitwa Lod kwenye Agano la Kale,na katika Israeli ya sasa.