sw_tn/act/05/38.md

20 lines
743 B
Markdown

# Sentensi unganishi:
Gamarieli anamaliza kuwaeleza wajumbe wa baraza. Pamoja na kuwapiga wale mitume na kuwaamuru wasizidi kunena habari za Yesu na kuwaachia huru, lakini wanafunzi walizidi kufundisha na kuhubiri habari za Yesu.
# jiepusheni na watu hawa na muwaache wenyewe,
Gamalieli anawaambia Wayahudi viongozi wasiwaadhibu hao mitume na wasiwatie tena gerezani.
# kama mpango huu au kazi hii ni ya watu itatupwa
Kama jambo hili wanalolitenda chimbuko lake ni mwanadamu litakoma tu.
# Lakini kama ni ya Mungu, hamtaweza kuwazuia
Kama kazi hii wanayoifanya chimbuko lake ni Mungu, kazi hii itaendelea.
# Hivyo, walishawishika na maneno yake.
Gamalieli alifanikiwa kuwashawishi Viongozi Wayahudi na kukubaliana na ushawishi wake.