sw_tn/2ki/19/16.md

837 B

Maelezo ya Jumla:

Mfalme Hezekia anaendelea kuomba kwa Yahwe baada ya kupokea barua kutoka kwa Mfalme Senakeribu wa Ashuru.

Tega sikio lako, Yahwe, na usikie. Fungua macho yako, Yahwe, na tazama

Sentensi hizi zote zinamsihi Yahwe kuvuta usikivu kwa vitu ambavyo Senakaribu anasema.

Tega sikio lako, Yahwe, na usikie

Maneno "Tega sikio lako" na "sikia" vinamaanisha kitu kimoja ni yanaongeza msisitizo kwenye maombi. "Yahwe, tafadhali sikiliza anachokisema."

Fungua macho yako, Yahwe, na ona

Maneno "Fungua macho yako" na "ona" yanamaanisha kitu kimoja na kuongeza msisitizo kwenye maombi. "Yahwe, tafadhali kuwa makini kwa kile kinachotokea."

Wameweka miungu yao kwenye moto

Wafalme wa Ashuru wamewachoma miungu ya mataifa mengine.

Waashuru wamewaangamiza

Waashuru wameiangamiza miungu yote ya mataifa na mataifa.