# Maelezo ya Jumla: Mfalme Hezekia anaendelea kuomba kwa Yahwe baada ya kupokea barua kutoka kwa Mfalme Senakeribu wa Ashuru. # Tega sikio lako, Yahwe, na usikie. Fungua macho yako, Yahwe, na tazama Sentensi hizi zote zinamsihi Yahwe kuvuta usikivu kwa vitu ambavyo Senakaribu anasema. # Tega sikio lako, Yahwe, na usikie Maneno "Tega sikio lako" na "sikia" vinamaanisha kitu kimoja ni yanaongeza msisitizo kwenye maombi. "Yahwe, tafadhali sikiliza anachokisema." # Fungua macho yako, Yahwe, na ona Maneno "Fungua macho yako" na "ona" yanamaanisha kitu kimoja na kuongeza msisitizo kwenye maombi. "Yahwe, tafadhali kuwa makini kwa kile kinachotokea." # Wameweka miungu yao kwenye moto Wafalme wa Ashuru wamewachoma miungu ya mataifa mengine. # Waashuru wamewaangamiza Waashuru wameiangamiza miungu yote ya mataifa na mataifa.