Mbinguni mara nyingi huelezewa kama mahali ambapo watu wanaimba.Hizo ni nyimbo za kumwabudu Mungu. Hii inaashiria kwamba mbinguni ni mahali ambapo Mungu anaabudiwa kila mara. (Tazama: [[rc://*/tw/dict/bible/kt/heaven]])
Sherehe za harusi ama karamu ni ishara muhimu inayotumika katika maandiko.Katika utamaduni wa Wayahudi, paradiso ama maisha pamoja na Mungu baada ya kifo ilipewa taswira ya karamu. Hapa Yesu anaipatia taswira ya karamu ya harusi ambayo mfalme huandalia mwana wake wa kiume ambaye ameoa sasa hivi. Mbali na hiyo, Yesu anasisitiza kwamba siyo watu wote Mungu hualika watajiandaa vilivyo ili washiriki. Watu kama hawa watatupwa nje ya karamu.