Matoleo mengine yanaweka maneno kulia kwa ukurasa kuliko maandishi mengine. ULB hufanya hivi na aya za 11-13 kuliko aya zingine. Huenda Paulo ananukuu shairi ama wimbo katika mistari hii.
Katika sura hii, Paulo anatumia mifano nyingi kufundisha maisha ya kikristo. Anatumia mifano ya mwanajeshi, mwanariadha na mkulima. Baadaye anatumia mifano ya aina nyingi ya vyombo vya nyumbani.