Kumjua Mungu inamaanisha kumilikiwa naye ama kuwa na uhusiano naye. Hapa "ujuzi" ni zaidi ya kumjua Mungu na akili. Ni ujuzu unaomfanya Mungu kumuokoa mtu na kumpa neema na amani. (Tazama: [[rc://*/tw/dict/bible/other/know]])
Petero anafundisha kwamba Mungu amewapa waumini yote wanayohitaji kuishi maisha ya kumcha Mungu. Kwa hivyo waumini wafanye kila waezalo kumtii Mungu zaidi. Waumini wakiendelea kufanya hivyo watakuwa imara na wenye manufaa kupitia uhusiano wao na Yesu. Lakini waumini wasipoendelea kuishi maisha ya kumcha Mungu, watakuwa ni kama wamesahau walichofanyiwa na Mungu kupitia kwa Kristo kuwaokoa. (Tazama: [[rc://*/tw/dict/bible/kt/godly]] and [[rc://*/tw/dict/bible/kt/save]])
Petero anafundisha kwamba unabii wa maandiko haukutolewa na binadamu. Roho Mtakatifu alifunua ujumbe wa Mungu kwa watu waliouandika kwa kitabu. Petero pia na Mitume wengine hawakubuni hadithi walizowapa watu kuhusu Yesu. Walishuhudia chenye Yesu alifanya na wakamsikia Mungu akimwita Yesu mwanawe.