sw_tn/psa/050/018.md

20 lines
839 B
Markdown
Raw Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# unakubaliana naye
Maana zinazowezekana ni 1) kwamba wanakubaliana na matendo ya mwizi. "unamkubali" au 2) kwamba wanamuunga mwizi katika matendo yake. "unamuunga"
# Unatoa mdomo wako kwa uovu
Mungu anamzungumzia mtu kuongea vitu vya uovu kana kwamba mdomo wa mtu ni mjumbe ambaye mtu anamtuma kufanya vitu viovu. "Daima huwa unasema vitu viovu"
# ulimi wako unaeleza uongo
Neno "ulimi" linawakilisha mtu anayezungumza. "huwa unasema uongo daima"
# Unakaa na kuzungumza dhidi ya ndugu yako; unamkashifu mtoto wa mama yako
Misemo hii miwili ina maana moja lakini inatumia maneno tofauti. Mungu anawashtaki kwa kuongea uongo dhidi ya watu wa familia yao wenyewe.
# Unakaa na kuzungumza
"Kukaa na kuzungumza" dhidi ya mtu inaashiria kuwa mtu huyu anawaza kwa makusudi vitu vibaya vya kusema kwa mtu. "Huwa unawaza namna ya kuongea"