# unakubaliana naye Maana zinazowezekana ni 1) kwamba wanakubaliana na matendo ya mwizi. "unamkubali" au 2) kwamba wanamuunga mwizi katika matendo yake. "unamuunga" # Unatoa mdomo wako kwa uovu Mungu anamzungumzia mtu kuongea vitu vya uovu kana kwamba mdomo wa mtu ni mjumbe ambaye mtu anamtuma kufanya vitu viovu. "Daima huwa unasema vitu viovu" # ulimi wako unaeleza uongo Neno "ulimi" linawakilisha mtu anayezungumza. "huwa unasema uongo daima" # Unakaa na kuzungumza dhidi ya ndugu yako; unamkashifu mtoto wa mama yako Misemo hii miwili ina maana moja lakini inatumia maneno tofauti. Mungu anawashtaki kwa kuongea uongo dhidi ya watu wa familia yao wenyewe. # Unakaa na kuzungumza "Kukaa na kuzungumza" dhidi ya mtu inaashiria kuwa mtu huyu anawaza kwa makusudi vitu vibaya vya kusema kwa mtu. "Huwa unawaza namna ya kuongea"