sw_tn/psa/046/010.md

20 lines
689 B
Markdown
Raw Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Kuwa kimya na ujue kuwa mimi ni Mungu
Hapa, Mungu anaanza kuzungumza.
# Kuwa kimya
Katika hali hii, maneno haya yanawezekana kuwa ni amri kwa mataifa kukomesha vita vyao. "Acheni kupigana"
# ujue kuwa mimi ni Mungu
Hapa neno "kujua" inamaanisha kuelewa na kukiri kuwa Yahwe ndiye Mungu wa kweli.
# Nitatukuzwa katika mataifa; nitatukuzwa duniani
Misemo hii miwili inamaana sawa na inasisitiza kuwa watu wa kila taifa duniani watamtukuza Mungu. "Watu katika kila taifa watanitukuza; watu duniani kote watanitukuza"
# Yahwe wa majeshi yuko nasi; Mungu wa Yakobo ni kimbilio letu
Mwandishi anamzungumzia Mungu kana kwamba ni sehemu ambayo watu wanaweza kwenda kwa ajili ya ulinzi.