# Kuwa kimya na ujue kuwa mimi ni Mungu Hapa, Mungu anaanza kuzungumza. # Kuwa kimya Katika hali hii, maneno haya yanawezekana kuwa ni amri kwa mataifa kukomesha vita vyao. "Acheni kupigana" # ujue kuwa mimi ni Mungu Hapa neno "kujua" inamaanisha kuelewa na kukiri kuwa Yahwe ndiye Mungu wa kweli. # Nitatukuzwa katika mataifa; nitatukuzwa duniani Misemo hii miwili inamaana sawa na inasisitiza kuwa watu wa kila taifa duniani watamtukuza Mungu. "Watu katika kila taifa watanitukuza; watu duniani kote watanitukuza" # Yahwe wa majeshi yuko nasi; Mungu wa Yakobo ni kimbilio letu Mwandishi anamzungumzia Mungu kana kwamba ni sehemu ambayo watu wanaweza kwenda kwa ajili ya ulinzi.