sw_tn/rev/19/11.md

37 lines
902 B
Markdown
Raw Normal View History

2018-04-12 01:01:04 +00:00
# Taarifa ya Jumla:
Hapa ni mwanzo wa maono mengine. Yohana anaanza kuelezea mpandaji wa farasi nyeupe.
# Kisha niliona mbingu zimefunguka
Hii picha inatumika kuashiria mwanzo wa maono mapya.
# yule aliyekuwa amempanda
Aliyempanda ni Yesu.
# Huhukumu kwa haki
Hapa "haki" inamaanisha kile kilicho sahihi. "Anahukumu watu wote kulingana na kile kilicho sahihi"
# Macho yake ni kama mwali wa moto
Yohana anazungumzia macho ya mpandaji kama vile yaling'aa kama mwali wa moto.
# jina lililoandikwa juu yake
Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mtu ameandika jina juu yake"
# asilolifahamu mtu yeyote isipokuwa yeye mwenyewe
"Yeye tu ndiye ajuae maana ya jina hilo"
# Amevaa vazi lililochovywa katika damu
Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Damu imefunika vazi lake"
# jina lake anaitwa Neno la Mungu
Unaweza kueleza hii kwa hali ya kutenda. "jina lake pia ni Neno la Mungu"