sw_tn/psa/143/007.md

36 lines
1.0 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# roho yangu ni dhaifu
"mimi ni mnyonge" au "nimekata tamaa sana"
# Usifiche uso wako kwangu
Hili ni ombi. "Nakuomba usijifiche kwangu" au "Tafadhali usijifiche kwangu"
# Usifiche uso wako kwangu
Mwandishi anamzungumzia Yahwe kukataa kufanya kile ambacho mwandishi wa zaburi anaomba kana kwamba Yahwe alikuwa anakataa hata kumtazama. "Usikatae kunisikiliza" au "Tafadhali nisikilize"
# Nitakuwa kama hao waendao shimoni
"Nitakuwa kama mtu mwingine tu aliyekufa"
# Acha nisikie uaminifu wako wa agano
"Nisababishe kusikia uaminifu wako wa agano" au "Niambie uaminifu wako wa agano"
# asubuhi
Maana zinazowezekana ni 1) asubuhi ni muda ambao watu wa wakati huo walidhani unafaa kuomba, au 2) "asubuhi kwa asubuhi," kila siku.
# Nioneshe
"Niambie"
# njia ninayopaswa kutembea
Mwandishi wa zaburi anazungumzia jinsi watu wanavyoishi kana kwamba ni njia ambayo wanatembea. "jinsi unavyotaka niishi"
# kwa kuwa ninainua roho yangu kwako
Maana zinazowezekana ni 1) "ninaomba kwako" au 2) "ninaamini kuwa utaniongoza na kunilinda"