# roho yangu ni dhaifu "mimi ni mnyonge" au "nimekata tamaa sana" # Usifiche uso wako kwangu Hili ni ombi. "Nakuomba usijifiche kwangu" au "Tafadhali usijifiche kwangu" # Usifiche uso wako kwangu Mwandishi anamzungumzia Yahwe kukataa kufanya kile ambacho mwandishi wa zaburi anaomba kana kwamba Yahwe alikuwa anakataa hata kumtazama. "Usikatae kunisikiliza" au "Tafadhali nisikilize" # Nitakuwa kama hao waendao shimoni "Nitakuwa kama mtu mwingine tu aliyekufa" # Acha nisikie uaminifu wako wa agano "Nisababishe kusikia uaminifu wako wa agano" au "Niambie uaminifu wako wa agano" # asubuhi Maana zinazowezekana ni 1) asubuhi ni muda ambao watu wa wakati huo walidhani unafaa kuomba, au 2) "asubuhi kwa asubuhi," kila siku. # Nioneshe "Niambie" # njia ninayopaswa kutembea Mwandishi wa zaburi anazungumzia jinsi watu wanavyoishi kana kwamba ni njia ambayo wanatembea. "jinsi unavyotaka niishi" # kwa kuwa ninainua roho yangu kwako Maana zinazowezekana ni 1) "ninaomba kwako" au 2) "ninaamini kuwa utaniongoza na kunilinda"