sw_tn/mat/11/23.md

48 lines
1.8 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2018-04-12 01:01:04 +00:00
# Sentensi unganishi:
Yesu anaendelea kukemea miji ambayo miujiza yake ilitendeka karibuni.
# Wewe, Kapernaum
Yesu sasa anaongea na watu wa mji wa Kapernaum kama vile walikuwa wanamsikiliza, lakini walikuwa hawasikilizi. Kiwakilishi ''wewe'' ni cha umoja kinarejelea Kapernaum kwa mistari yote miwili.
# wewe
Matukio yote ya kiwakilishi cha "wewe" yakao katika umoja. Kama kinatumika kila mahali kuonyesha watu wa mji, basi kiwakilishi cha wewe kitafsiriwe katika wingi wake
# Kapernaum...Sodoma
Majina ya miji hii yametumika kumaanisha watu waliokuwa wanaishi Kapernaum na Sodoma.
# unadhani utainuliwa hadi mbinguni?
"unadhani utainuliwa hadi mbinguni ?" Yesu anatumia balagha kuwakemea watu wa Kapernaum kwa majivuno yao. "inaweza pia kutumika kwa mfumo tendaji. "huwezi kujiinua mwenyewe hadi mbinguni" au "sifa za watu wengine haziwezi kukuinua hadi mbinguni kama unavyodhani atafanya"
# utashuswa hadi chini kuzimu
Hii inaweza kuelezwa katika mfumo tendaji ''Mungu atakupeleka hadi kuzimu.''
# Kama katika Sodoma ... ingekuwepe hadi leo
Yesu anatumia mazingira ya kubuni ambayo yangetokea katika siku zilizopita, lakini haikutokea.
# matendo makuu
''''matendo makuu'' au ''kazi ya nguvu za Mungu'' au "miujiza"
# ingekuwepo hadi leo
Kiwakilishi ''inge'' kinarejelea kwa mji wa Sodoma
# nasema kwako
Kirai hiki kinaongeza msisitizo wa kile Yesu alichosema baadaye
# itakuwa rahisi kwa nchi ya Sodoa kusimama katika siku ya hukumu kuliko wewe
Hapa "nchi ya Sodoma" inamaansha watu walioishi kule. ''Mungu ataonyesha rehema kwa watu wa Sodoma katika siku ya hukumu kuliko kwako'' au Mungu atawapa adhabu kali zaidi katika siku ya hukumu kuliko watu wa Sodoma.''
# kuliko wewe
Taarifa zilizofumbwa ziwekwe wazi. "kwa sababu haukutubu na kuniamini, ingawa uliniona nikifanya miujiza"