sw_tn/mat/01/22.md

28 lines
814 B
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2018-04-12 01:01:04 +00:00
# Taarifa kwa ujumla
Mwandishi amnukuu nabii Isaya kuonesha kwamba kuzaliwakwa Yesu kulikuwa kwa mujibu wa andiko
# Hii yote ilitokea
Malaika hazungumzi tena. Mathayo sasa anaeleza umuhimu wa kile malaika alikisema.
# kilichonenwa na Bwana kwa njia ya nabii
Hii inaweza kuelezwa kwa namna iliyo tendaji. "kile ambacho Bwana alimwambia nabii Isaya kuandika zamani."
# Tazama...Emanueli
Hapa Mathayo anamnukuu nabii Isaya.
# Tazama
Neno hili huongeza msisitizo kwa kile kilicho fuata kusemwa. "Tazama" au "Sikia" au "Kuwa makini kwa kile ninachotaka kukuambia"
# Emanueli
Hili ni jina la kiume.
# maana yake 'Mungu pamoja nasi'
Hii haimo katika kitabu cha Isaya. Mathayo anaeleza maana ya jina "Emanueli." Unaweza kulitafsiri kama sentenso iliyo peke yake. "Jina hili maana yake 'Mungu pamoja nasi.'"