sw_tn/isa/47/06.md

28 lines
1020 B
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Kauli Kiunganishi
Yahwe anaendelea kuzungumza na Babeli kuhusu anguko lake kana kwamba alikuwa malkia ambaye ameaibishwa.
# Nilikasirishwa
Hapa "nilikasirishwa" ina maana ya Yahwe.
# nilitia unajisi urithi wangu
Yahwe anazungumzia watu wa Israeli kuwa milki yake maalumu kana kwamba walikuwa urithi wake. "Niliwanajisi watu wangu, ambao walikuwa milki yangu maalumu"
# kuwakabidhi mikononi mwako
Hapa neno "mkononi" inawakilisha nguvu na utawala wa Babeli. "Ninawaweka chini ya nguvu yako"
# umeweka nira nzito sana juu ya watu wazee
Yahwe anazungumzia Wababeli kuwakandamiza watu wazee kana kwamba wamewatendea watu wazee kama ng'ombe na kuweka nira nzito juu ya shingo zao.
# nitatawala milele kama malkia wa enzi
Babeli inazungumzia kutawala kwa kudumu juu ya mataifa mengi kana kwamba ilikuwa malkia ambaye atatwala milele.
# Hukuviweka vitu hivi moyoni
Yahwe anazungumzia juu ya kufikiria kwa makini kuhusu kitu kana kwamba ilikuwa ni kuweka kitu hicho ndani ya moyo wa mtu. "Haukufikiria vitu hivi"