# Kauli Kiunganishi Yahwe anaendelea kuzungumza na Babeli kuhusu anguko lake kana kwamba alikuwa malkia ambaye ameaibishwa. # Nilikasirishwa Hapa "nilikasirishwa" ina maana ya Yahwe. # nilitia unajisi urithi wangu Yahwe anazungumzia watu wa Israeli kuwa milki yake maalumu kana kwamba walikuwa urithi wake. "Niliwanajisi watu wangu, ambao walikuwa milki yangu maalumu" # kuwakabidhi mikononi mwako Hapa neno "mkononi" inawakilisha nguvu na utawala wa Babeli. "Ninawaweka chini ya nguvu yako" # umeweka nira nzito sana juu ya watu wazee Yahwe anazungumzia Wababeli kuwakandamiza watu wazee kana kwamba wamewatendea watu wazee kama ng'ombe na kuweka nira nzito juu ya shingo zao. # nitatawala milele kama malkia wa enzi Babeli inazungumzia kutawala kwa kudumu juu ya mataifa mengi kana kwamba ilikuwa malkia ambaye atatwala milele. # Hukuviweka vitu hivi moyoni Yahwe anazungumzia juu ya kufikiria kwa makini kuhusu kitu kana kwamba ilikuwa ni kuweka kitu hicho ndani ya moyo wa mtu. "Haukufikiria vitu hivi"