sw_tn/isa/30/20.md

32 lines
920 B
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Taarifa ya Jumla
Isaya anaendelea kuzungumza na watu wa Yuda.
# mkate wa shida na maji ya mateso
Hapa "mkate" na "maji" huunda mlo wa mtu maskini sana. Msemo wote unawakilisha nyakati ngumu na umaskini wa watu.
# mwalimu wako
Hii ina maana ya Yahwe.
# utamwona mwalimu wako kwa macho yako mwenyewe
Hapa "macho" inawakilisha mtu mzima. "nyie wenyewe mtamwona mwalimu wenu"
# Masikio yako yatasikia
Hapa "masikio" inawakilsha mtu mzima. "Utasikia"
# neno nyuma yako likisema
Hapa "neno" linawakilisha mtu anayezungumza. "yule anayezungumza nyuma yako akisema"
# Hii ndiyo njia, tembea juu yake
Jinsi Yahwe anavyotaka watu wake kuenenda inazungumziwa kana kwamba ilikuwa njia au barabara. Kumtii Yahwe inazungumziwa kana kwamba ilikuwa mtu akitembea katika njia yake.
# utakapogeuka kulia au utakapogeuka kushoto
Kumkaidi Yahwe inazungumziwa kana kwamb mtu aligeuka kushoto au kulia katika njia ya Yahwe.