# Taarifa ya Jumla Isaya anaendelea kuzungumza na watu wa Yuda. # mkate wa shida na maji ya mateso Hapa "mkate" na "maji" huunda mlo wa mtu maskini sana. Msemo wote unawakilisha nyakati ngumu na umaskini wa watu. # mwalimu wako Hii ina maana ya Yahwe. # utamwona mwalimu wako kwa macho yako mwenyewe Hapa "macho" inawakilisha mtu mzima. "nyie wenyewe mtamwona mwalimu wenu" # Masikio yako yatasikia Hapa "masikio" inawakilsha mtu mzima. "Utasikia" # neno nyuma yako likisema Hapa "neno" linawakilisha mtu anayezungumza. "yule anayezungumza nyuma yako akisema" # Hii ndiyo njia, tembea juu yake Jinsi Yahwe anavyotaka watu wake kuenenda inazungumziwa kana kwamba ilikuwa njia au barabara. Kumtii Yahwe inazungumziwa kana kwamba ilikuwa mtu akitembea katika njia yake. # utakapogeuka kulia au utakapogeuka kushoto Kumkaidi Yahwe inazungumziwa kana kwamb mtu aligeuka kushoto au kulia katika njia ya Yahwe.