sw_tn/isa/03/18.md

52 lines
1.3 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Taarifa ya Jumla
Hii inaendelea kumfafanua jinsi Yahwe atakavyohukumu wanawake wa Yerusalemu.
# Bwana ataondoa
Hapa "ataondoa" inawakilisha kusababisha wengine kuondoa kitu. "Bwana atasababisha wengine kuondoa"
# mapambo ya vito vya kifundo cha mguu
Pambo ambalo wanawake huvaa katika kifundo cha miguu, juu kidogo ya mguu.
# ukanda wa kichwani
Pambo ambalo wanawake huvaa juu ya vichwa na nywele
# mapambo yenye umbo la mwezi mwandamo
Mapambo yenye umbo la mwezi ambao watu huvaa kwa imani ya kwamba yatamlinda mtu kutoka na uovu.
# lozi ya kidani ya sikioni
mapambo ya vito ambayo huning'inia kutoka kwenye sikio au juu ya sikio
# bangili
Pambo ambalo wanawake huvaa katika mikono
# shela
nyenzo nyembamba sana inayotumika kufunika kichwa na uso wa mwanamke
# hijabu
vipande vyembamba vya nguo, virefu ambavyo wanawake hujifunga kuzunguka kichwa au nywele.
# mkufu wa kifundo cha mguu
Haya ni mapambo ambayo wanawake huvaa karibu na miguu. Mara kwa mara mikufu huning'inia chini na kutoa sauti ya chini.
# mishipi
kipande cha nguo ambacho watu huvaa kuzunguka kiuno au kupita kifuani.
# visanduku vya manukato
kisanduku kidogo au mfuko unaokuwa na manukato ambayo wanawake walivaa juu ya mikufu au kamba kuzunguka shingo zao ili watoe harufu nzuri.
# hirizi ya bahati
mapambo ya vito ambayo watu huvaa kwa imani ya kwamba italeta bahati nzuri