# Taarifa ya Jumla Hii inaendelea kumfafanua jinsi Yahwe atakavyohukumu wanawake wa Yerusalemu. # Bwana ataondoa Hapa "ataondoa" inawakilisha kusababisha wengine kuondoa kitu. "Bwana atasababisha wengine kuondoa" # mapambo ya vito vya kifundo cha mguu Pambo ambalo wanawake huvaa katika kifundo cha miguu, juu kidogo ya mguu. # ukanda wa kichwani Pambo ambalo wanawake huvaa juu ya vichwa na nywele # mapambo yenye umbo la mwezi mwandamo Mapambo yenye umbo la mwezi ambao watu huvaa kwa imani ya kwamba yatamlinda mtu kutoka na uovu. # lozi ya kidani ya sikioni mapambo ya vito ambayo huning'inia kutoka kwenye sikio au juu ya sikio # bangili Pambo ambalo wanawake huvaa katika mikono # shela nyenzo nyembamba sana inayotumika kufunika kichwa na uso wa mwanamke # hijabu vipande vyembamba vya nguo, virefu ambavyo wanawake hujifunga kuzunguka kichwa au nywele. # mkufu wa kifundo cha mguu Haya ni mapambo ambayo wanawake huvaa karibu na miguu. Mara kwa mara mikufu huning'inia chini na kutoa sauti ya chini. # mishipi kipande cha nguo ambacho watu huvaa kuzunguka kiuno au kupita kifuani. # visanduku vya manukato kisanduku kidogo au mfuko unaokuwa na manukato ambayo wanawake walivaa juu ya mikufu au kamba kuzunguka shingo zao ili watoe harufu nzuri. # hirizi ya bahati mapambo ya vito ambayo watu huvaa kwa imani ya kwamba italeta bahati nzuri