Watafsiri wengine wamewaka kila msitari wa ushairi kulia kuliko maandishi mengine ili isomeke kwa urahisi. ULB inafanya hivi na ushairi katika 3:7-11,15, ambayo ni maneno kutoka Agano la Kale.
Mwandishi anatumia maswali ya hadithi kama njia ya kuwaonya wasomaji wake. Yeye pamoja na wasomaji wake wanajua majibu ya maswali haya na mwandishi anajua kwamba wakati wasomaji watafikiria juu ya majibu ya haya maswali, watatambua kwamba wanatakikana kumsikiliza Mungu na kumtii.