sw_tn/gen/43/21.md

40 lines
1.1 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Kauli Kiunganishi:
Ndugu wanaendelea kuzungumza na mtunzaji wa nyumba.
# Ikawa
Msemo huu unatumika kuweka alama ya tukio muhimu la simulizi.
# tulipofika katika eneo la kupumzikia
"tulipofika mahali ambapo tulikwenda kukaa usiku ule"
# tazama
Neno "tazama" hapa linaonyesha ya kwamba ndugu walishangazwa kwa kile walichokiona.
# pesa ya kila mtu ilikuwa katika gunia lake, pesa yetu kwa kiasi kamili
"kila mmoja wetu alikuta pesa kamili katika gunia lake"
# Tumeileta katika mikono yetu.
Hapa "mikono" ina maana ya mtu mzima. "Tumerudisha pesa pamoja nasi"
# Tumekuja na pesa nyingine pia mikononi mwetu ili kununua chakula
Hapa "mikono" ina maana ya mtu mzima. "Tumekuja na pesa zaidi pia kununua chakula zaidi"
# Tumekuja na
Ilikuwa kawaida kutumia msemo "kushuka" pale ambapo inazungumziwa safari ya kutoka Kaanani kwenda Misri.
# Amani iwe kwenu
Nomino inayojitegemea "Amani" inaweza kuwekwa kama kitenzi. "Tulia" au "Tulieni"
# Mungu wenu na Mungu wa baba yenu
Mtunzaji hazungumzi kuhusu Mungu wawili tofauti. "Mungu wenu, Mungu ambaye baba yenu anamwabudu"