# Kauli Kiunganishi: Ndugu wanaendelea kuzungumza na mtunzaji wa nyumba. # Ikawa Msemo huu unatumika kuweka alama ya tukio muhimu la simulizi. # tulipofika katika eneo la kupumzikia "tulipofika mahali ambapo tulikwenda kukaa usiku ule" # tazama Neno "tazama" hapa linaonyesha ya kwamba ndugu walishangazwa kwa kile walichokiona. # pesa ya kila mtu ilikuwa katika gunia lake, pesa yetu kwa kiasi kamili "kila mmoja wetu alikuta pesa kamili katika gunia lake" # Tumeileta katika mikono yetu. Hapa "mikono" ina maana ya mtu mzima. "Tumerudisha pesa pamoja nasi" # Tumekuja na pesa nyingine pia mikononi mwetu ili kununua chakula Hapa "mikono" ina maana ya mtu mzima. "Tumekuja na pesa zaidi pia kununua chakula zaidi" # Tumekuja na Ilikuwa kawaida kutumia msemo "kushuka" pale ambapo inazungumziwa safari ya kutoka Kaanani kwenda Misri. # Amani iwe kwenu Nomino inayojitegemea "Amani" inaweza kuwekwa kama kitenzi. "Tulia" au "Tulieni" # Mungu wenu na Mungu wa baba yenu Mtunzaji hazungumzi kuhusu Mungu wawili tofauti. "Mungu wenu, Mungu ambaye baba yenu anamwabudu"