sw_tn/gen/41/50.md

36 lines
871 B
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Kabla miaka ya njaa kuingia
Hii inazungumzia kuhusu miaka saba kana kwamba ni kitu kinachosafiri na kuja kutulia mahali. "kabla ya miaka saba ya njaa kuanza"
# Asenathi
"Asenathi" ni jina la mwanamke ambaye Faro alimpatia Yusufu kama mke wake.
# binti wa Potifera
"Potifera" ni baba wa Asenathi.
# kuhani wa Oni
Oni ni mji, ambao pia unajulikana kama Heliopolisi, ambao ulikuwa "Mji wa Jua" na makao ya kumuabudu mungu wa jua Ra.
# Manase
"Jina la 'Manase' lina maana ya "kusababisha kusahau""
# nyumba ya baba yake
Hii ina maana ya baba wa Yusufu Yakobo na familia yake.
# Efraimu
"Jina la 'Efraimu' lina maana ya 'kuwa na uzao' au 'kupata watoto'"
# amenipa uzao
Hapa "uzao" ina maana ya kufanikiwa au kupata watoto.
# katika nchi ya mateso yangu
Nomino inayojitegemea "mateso" inaweza kuwekwa kama "nimeteseka". "katika nchi hii ambayo nimeteseka".