# Kabla miaka ya njaa kuingia Hii inazungumzia kuhusu miaka saba kana kwamba ni kitu kinachosafiri na kuja kutulia mahali. "kabla ya miaka saba ya njaa kuanza" # Asenathi "Asenathi" ni jina la mwanamke ambaye Faro alimpatia Yusufu kama mke wake. # binti wa Potifera "Potifera" ni baba wa Asenathi. # kuhani wa Oni Oni ni mji, ambao pia unajulikana kama Heliopolisi, ambao ulikuwa "Mji wa Jua" na makao ya kumuabudu mungu wa jua Ra. # Manase "Jina la 'Manase' lina maana ya "kusababisha kusahau"" # nyumba ya baba yake Hii ina maana ya baba wa Yusufu Yakobo na familia yake. # Efraimu "Jina la 'Efraimu' lina maana ya 'kuwa na uzao' au 'kupata watoto'" # amenipa uzao Hapa "uzao" ina maana ya kufanikiwa au kupata watoto. # katika nchi ya mateso yangu Nomino inayojitegemea "mateso" inaweza kuwekwa kama "nimeteseka". "katika nchi hii ambayo nimeteseka".